Kirinyaga: OCS Harrison Muteti aaga dunia kwenye ajali mbaya ya barabarani

August 2024 ยท 1 minute read

Harrison Muteti Katecho ambaye ni afisa mkuu (OCS) wa kituo cha polisi cha Warungu kunti ya Kirinyaga ameaga dunia.

Katecho alipoteza maisha yake baada ya gari alilokuwa akiendesha kuligonga lori lililokuwa limeegeshwa kando ya barabara eneo la Kamakis, Eastern Bypass, Ruiru.

Habari Nyingine: Bintiye Gavana Obado ana kiburi, awaonesha Wakenya ishara chafu ya kidole

Kulingana na maafisa wa polisi, ajali hiyo iliyotokea Jumatano, Agosti 26, OCS huyo alishindwa kulidhibiti gari lake la Toyota Belta na kuligonga lori hilo.

Afisa huyo alipata majeraha kichwani na kifuani wakati wa ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tisa jioni.

"Magari yote mawili yalikuwa yanaelekea upande wa Ruai kwenye barabara ya Thika wakati dereva wa gari dogo kiutokana na sababu ambazo hazijajulikana alipoteza mwelekeo na kuligonga lori," ripoti ya polisi ilisema.

Habari Nyingine: Baba halali wa mtoto wa Jowie ajitokeza, adai binti ni wake

Katecho alithibitishwa kuwa alikuwa ameaga dunia alipofikishwa katika hospitali ya eneo bunge la Ruiru alipokimbizwa kwa matibabu.

Mwili wake ulipelekwa katika makafani ya Chuo Kikuu cha Kenyatta huku gari lake likipelekwa katika kituo cha polisi cha Ruiru.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbIN2fpZmoqKqmaPGorPAZqacq12drrO%2ByKymp2WdqsGmwMhmmJqfkWKxtrrImmSkr5WjxqZ5wKOYpaFdoq%2BixcBmsJplkpa%2Foq7Aq5inoV6dwa64